Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua".
Imepokelewa na Imamu Muslim
Ufafanuzi
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kumtaja Allah Mtukufu kwa maneno haya matukufu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na utajo huo ni kusema:
"Sub-haana llaah": Ni kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na mapungufu.
"Alhamdulillaah": Ni kumsifia kwa sifa za ukamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza.
"Laa ilaaha illa llaah": Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu.
"Allaahu Akbaru: Mkubwa na Mtukufu kuliko kila kitu.
Hadeeth benefits
Himizo la kumtaja Mwenyezi Mungu, nakuwa hilo linapendeka zaidi kuliko vyote vilivyochomozewa na jua.
Himizo la kukithirisha dhikiri; kwakuwa ndani yake kuna malipo na fadhila kubwa.
Starehe za dunia ni ndogo na matamanio yake ni yenye kuondoka.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others