- Malipo haya anayapata atakayelisema neno hilo ndani ya siku nzima mfululizo au kwa nyakati tofauti tofauti.
- Tasbihi: Ni kumtakasa Allah kutokana na mapungufu, na kumhimidi: Ni kumsifu kwa ukamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza.
- Makusudio katika hadithi hii ni kufutwa madhambi madogo madogo, ama madhambi makubwa haya ni lazima yafanyiwe toba.