- Kutofauti watu katika swala la imani.
- Inapendeza kuwa na nguvu katika matendo; kwani hupatikana faida kwa matendo hayo ambayo haipatikani kukiwa na udhaifu.
- Mwanadamu anatakiwa apupie katika yale yenye kumnufaisha, na aache yasiyomnufaisha.
- Ni wajibu kwa muumini atake msaada wa Mwenyezi Mungu kwake katika mambo yake yote, na wala asiitegemee nafsi yake.
- Kuthibiti uwepo wa mipango na maamuzi ya Mwenyezi Mungu (kadhaa na kadari), nakuwa hilo halipingani na swala la mtu kufanya sababu na kwenda kutafuta mambo mazuri na ya kheri.
- Katazo la kusema: "Lau" kwa njia ya kulalamika wakati wa kupatwa na mitihani, na uharamu wa kupingana na maamuzi na mipango ya Allah Mtukufu.