- Pupa ya Masahaba katika kuyajua mambo yenye manufaa katika Dunia na Akhera.
- Salamu na kulisha chakula ni miongoni mwa amali bora katika Uislamu; kwa sababu ya fadhila zake na uhitaji wa watu juu ya chakula katika wakati wote.
- Kwa mambo haya mawili ihisani (wema) unakuwa kwa kauli na vitendo, nao ndio wema uliokamilika zaidi.
- Mambo haya ni katika mambo yanayohusu maisha ya waislamu baina yao, na kuna mambo yanahusu mahusiano ya mja na Mola wake.
- Kuanza kwa salamu ni maalumu kwa waislamu, haitolewi salamu kwa kumuanza asiyekuwa muislamu.