- Ukamilifu wa Uislamu hauwi isipokuwa kwa kutofanyia maudhi watu wengine, kwa vitendo au kwa hila yoyote.
- Ametaja ulimi na mkono pekee pasina viungo vingine; kwa sababu ya wingi wa makosa yake na madhara yake, kwani shari nyingi hutokea kupitia viwili hivi.
- Himizo la kuacha maasi na kushikamana na yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Muislamu bora kuliko wote ni yule mwenye kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waislamu.
- Uadui unaweza kuwa kwa kauli au kitendo.
- Kuhama kuliko kamilika ni kuyahama aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.