- Dini ya Uislamu ni dini ya huruma, na dini nzima imesimama katika kumtii Mwenyezi Mungu na kuwatendea wema viumbe.
- Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka anasifika kwa sifa ya huruma, naye Mtukufu ni Mwingi wa rehema mwenye kurehemu, mfikishaji wa huruma kwa waja wake.
- Malipo huendana na matendo, wenye huruma huwahurumia Rahman -Mwingi wa rehema-.