- Huruma inahitajika kwa viumbe wote, lakini wametajwa watu kama sehemu ya kuwapa kipaumbele.
- Mwenyezi Mungu ndiye Mwingi wa huruma na anawahurumia waja wake wenye huruma, kwani malipo huendana na matendo.
- Huruma kwa watu inakusanya kuwafikishia kheri na kuwazuilia shari na kuamiliana nao kwa wema.