- Ukweli ni tabia adhimu ambayo hupatikana kupitia juhudi, kwa sababu mtu anapoendelea kuwa mkweli na kuutafuta ukweli, mpaka ukweli unakuwa ni kama tabia yake ya asili, basi huandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni miongoni mwa wa watu wakweli na wema.
- Uongo ni tabia ya kulaumiwa ambayo mhusika huipata kupitia mazoea ya muda mrefu katika maneno na matendo, mpaka inakuwa ni tabia na silika yake, kisha anaandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni katika waongo.
- Ukweli unahusu ukweli wa ulimi, ambao ni kinyume cha uongo, na ukweli katika nia, ambao ni ikhlasi, na ukweli katika kusuluhisha vyema nia yake, na ukweli katika vitendo, na kwa uchache zaidi ni siri yake na dhahiri yake viwe sawa, na ukweli katika matukio kama kusema ukweli wakati wa hofu na raha, na mengineyo, hivyo yeyote atakayesifika na sifa hizo basi atakuwa ni mkweli mno, au akasifika na baadhi yake atakuwa mkweli pia.