- Himizo la kusaidizana na kuhurumiana na kutatua haja za watu madhaifu.
- Ibada inakusanya kila amali njema, na miongoni mwa ibada ni kwenda haraka kuwasaidia wajane na masikini.
- Amesema Bin Hubaira: Na makusudio yake hapa nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu humkusanyia thawabu za mfungaji na msimamaji usiku kwa ajili ya ibada na mpigana Jihadi kwa mpigo mmoja; na hii ni kwa sababu amesimama na mjane nafasi ya mume wake..., na akasimama upande wa masikini aliyeshindwa kujimudu mwenyewe, akatoa hiki kilichozidi katika matumizi yake, na akatoa sadaka kwa kuikandamiza nafsi yake, ndio maana manufaa yake yakawa sawa na swaumu na kisimamo cha usiku na Jihadi.