- Amesema bin Daqiiq Al-Idd: Hadithi hii ni tukufu mno, imekusanya aina mbali mbali za elimu na kanuni na adabu, ndani yake kuna fadhila za kukidhi haja za waislamu na kuwanufaisha kwa kadiri ya uwezo, kama elimu, au mali, au msaada, au kumuelekeza katika masilahi, na nasaha, au mengineyo.
- Himizo la kumfanyia wepesi mwenye hali ngumu.
- Himizo la kumsaidia mja muislamu, nakuwa Mwenyezi Mungu anamsaidia mwenye kusaidia kulingana na masada wake kwa ndugu yake.
- Miongoni mwa kumsitiri muislamu: Ni kutochunguza aibu zake, na imepokelewa kutoka kwa mmoja kati ya wema waliotangulia alisema kuwa: Niliishi na watu hawakuwa na aibu, waliposema aibu za watu, na watu wakasema aibu zao, na niliishi na watu hawakuwa na aibu, wakajizuia kuzungumza aibu za watu, zikasahaulika aibu zao.
- Si katika kuwasitiri watu kuacha uovu utendeke na kutoukemea, bali anaukemea na anasitiri, na hii ni kwa yule ambaye hajulikani kwa uovu na kuendelea katika ujeuri, na ama mwenye kufahamika kwa uovu, huyu hastahiki kusitiriwa, bali swala lake linafikishwa kwa mwenye mamlaka, kama hatohofia madhara kwa hilo; na hii ni kwa sababu kumsitiri kunamhadaa ili aendelee kuwaudhi watu, na anampa ujasiri mwingine katika watu wa shari na ukaidi.
- Himizo la kutafuta elimu na kusoma Qur'ani na kujifunza.
- Amesema Nawawi: Katika hili kuna dalili ya ubora wa kukusanyika katika kuisoma Qur'ani msikitini...na kunaunganishwa na msikiti katika fadhila hizi kukusanyika katika madrasa, na jihadi, na mfano wake, in shaa Allah.
- Malipo Mwenyezi Mungu ameyaweka katika matendo na si katika ukoo.