- Muundo wa mifupa na viungo vya mwanadamu ni moja ya neema kubwa za Mwenyezi Mungu juu yake, hivyo kila mfupa peke yake unahitaji kutolewa sadaka kwa niaba yake ili itimie kushukuru neema hiyo.
- Himizo la kurudia upya shukurani kila siku ili neema hizo zidumu.
- Himizo la kudumu kufanya ibada za sunna na sadaka kila siku.
- Fadhila ya kusuluhisha baina ya watu.
- Himizo la mtu kumsaidia ndugu yake; kwani msaada wake kwake ni sadaka.
- Himizo la kuhudhuria swala za pamoja na kuziendea, na kuimarisha misikiti kwa hilo.
- Uwajibu wa kuheshimu njia wanazopita waumini kwa kuepuka yanayo waudhi au kuwadhuru.