- Ubora wa mapenzi ya dhati yanayokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, si kwa ajili ya masilahi ya kidunia.
- Inapendeza na ni sunna kumueleza anayependwa kwa ajili ya Allah, ili kuongeza mapenzi na kuzoeana.
- Kuenea kwa mapenzi baina ya waumini hutia nguvu udugu wa kiimani na huhifadhi jamii kuto pasuka na kufarakana.