- Kumebainishwa baadhi ya alama za mnafiki na tahadhari ya kutoangukia katika unafiki.
- Makusudio ya hadithi: Ni kuwa sifa hizi ni sifa za unafiki, na mwenye sifa hizi anafanana na wanafiki kwa sifa hizi, na amejipamba kwa tabia zao, haina maana kuwa ni mnafiki anayedhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri, na wamesema baadhi ya wanachuoni kuwa hii inachukuliwa kwa mtu ambaye zitakuwa nyingi kwake sifa hizi na akazipuuzia, na akaziona ndogo; basi atakayekuwa hivyo mara nyingi huwa kaharibika katika itikadi yake.
- Amesema Imam Ghazal: Msingi wa dini zote umekusanywa na mambo matatu: Kauli, kitendo, na nia, akatanabahisha kuwa kuharibika kwa maneno ni kwa uongo, na kuharibika kwa vitendo kunakuwa kwa hiyana, na kuharika kwa nia ni kwa kwenda kinyume; kwa sababu kwenda kinyume na ahadi hakumchafui mtu isipokuwa maazimio yake yatakapoambatanishwa na ahadi, ama atakapokusudia kisha kikamtokea kizuizi au akabadili mtazamo huyu hatokuwa na sura ya unafiki.
- Unafiki una aina mbili: Unafiki wa kiitikadi unamtoa mtu katika imani, nao ni kudhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri, na unafiki wa vitendo, nao ni kujifananisha na wanafiki katika tabia zao, na huu haumtoi mtu katika imani, isipokuwa ni dhambi katika madhambi makubwa.
- Amesema bin Hajari: Na wamekubaliana wanachuoni kuwa atakayesadikisha kwa moyo wake na ulimi wake na akafanya mambo haya hahukumiwi kwa ukafiri, wala si mnafiki atakayekaa motoni milele.
- Amesema Imam Nawawi: Na wamesema wanachuoni wengi kuwa: Makusudio yake ni wanafiki waliokuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake walizungumza kwa imani yao, na wakapinga, na wakaaminiwa kwa dini yao wao wakafanya hiyana, na wakaahidi katika swala la dini na kuinusuru, wakaenda kinyume, na wakavuka mipaka katika ugomvi wao.