- Fadhila za upole na kudhibiti nafsi wakati wa hasira, nakuwa hili ni katika matendo mema ambayo uislamu umeyahimiza.
- Kupambana na nafsi wakati wa hasira ni zaidi ya kupambana na adui.
- Uislamu umebadili mtazamo wa nguvu wa enzi za ujinga kuwa ni tabia njema, hivyo, mtu mwenye nguvu zaidi kuliko wote ni yule mwenye kumiliki uongozi wa nafsi yake.
- Kujiweka mbali na hasira; kwani husababisha madhara kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii nzima kwa ujumla.