- Tahadhari dhidi ya hasira na sababu zake, kwani ndio chanzo kikuu cha shari, na kujikinga nayo ni chanzo cha kheri.
- Kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama kuchukia wakati yanapofanyika maharamisho yake ni miongoni mwa hasira nzuri.
- Kurudia maneno wakati wa haja mpaka ayaelewe msikilizaji na atambue umuhimu wake.
- Ubora wa kuomba usia kutoka kwa msomi.