- Katazo la kulipiza kwa zaidi ya vile ulivyofanyiwa.
- Mwenyezi Mungu hakuwaamrisha waja wake lolote lenye kuwadhuru.
- Katazo la kujidhuru au kudhuru ima kwa kauli au kitendo au kuacha.
- Malipo hulingana na kitendo, atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakaye tia ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtia ugumu.
- Katika kanuni za sheria: Ni "Madhara huondoshwa", Hivyo, sheria haikubaliani na madhara, na inakataza kujidhuru.